Kwa Mkongo Queens Ndo Tunaanza Ligi Sasa - Saidi P

Leo Feb 03, 2018.

Meneja wa team ya Kwa Mkongo Queens,Said P amefunguka na kusema ndo kwanza  wanaanza ligi sasa ivyo wapinzani wajiandae kwa kila atakae karibia ni kichapo tu,licha ya kupoteza mechi mbili,moja nyumbani na moja ugenini,ambapo mechi ya nyumbani walifugwa bao 4-0 dhidi ya Msufini na mechi ya ugenini walifugwa bao 2_1 dhidi ya Saku.

Ameyasema hayo wakati alipo kuwa kwenye maandalizi ya mchezo wao wa leo jumamosi dhidi ya Dovya B utakao chezwa kwenye uwanja wao Kwa mkongo.

"tumejipanga na mmechezo wetu wa hapo jumamosi, utakuwa ni mchezo wa kujiuliza kwa michezo yetu miwili tulio poteza,kwetu sisi huu mchezo wa jumamosi ndo kama  tunaanza ligi" amesema Said P.

Licha ya hayo Said P aliendelea kwa kuwakaribisha wadau na wapenzi wote wa mchezo wa rede.

"nipenda tu kuwakaribisha wadau wote waje kuona maboresho ya kikosi chetu na kuona wachezaji wadogo wenye uwezo wa kuimili mipira vizuri" amesema Said P.

Maoni