Kwa Mkongo Queens Yawafungia wachazaji watano kwa utovu wa nidhamu

Uongozi wa Klabu ya Kwa Mkongo Queens,umewafungia wachazaji watano,Zubeda Ally, Ratifa Mohamed, Aisha Juma ,Zulfa Gulam na Amini Salehe  kutokana na utovu wa nidhamu walio uwonesha kwenye mchezo wao dhidi ya Dovya A.

Akithibitisha Taarifa za kuwafungia wachezaji hao Mwenyekiti wa Klabu Said P amesema wachezaji hao wamefanya kitendo ambacho kama watasita kuwaadhibu basi watapandikiza tabia mbaya kwa wachezaji wengne.

"Wamefanya kosa kubwa sana na si la kuvumilika,kwani kwenye michezo lugha za matusi hazipendezi na hazina nafasi na walio tolewa lugha izo chafu ni viongozi wetu wakubwa na tunawaheshimu sana na wachezaji wa upande wa pili,ivyo tunawafungia mechi 5 kila moja na hawatoshiriki safari yoyote katika chama na jumuhiya kwa ujumla adi watakapojirekebisha tabia zao" Amesema Said P.

Said P pia amesema wachazaji hao tayari wamekwisha kuandika barua ya kuomba radhi kutokana na kitendo walichokifanya.

"Bahati nzuri wamekiri makosa  yao na nimewambia kila mmoja andike barua ya kuomba radhi na pia nitawaomba viongozi wangu walio fanyiwa kitendo iko cha utovu wa nidhamu akiwepo Mwenyekiti wangu wa Umoja wa vijana kata ya chamazi,Nasri Mkalipa na Katibu wake Juma Bega ili kuwaomba radhi kwa ili. Amesema Said P. 

Mpaka sasa Kwa Mkongo  Queens wamesaliwa na michezo 2 kabla ya mzunguko wa kwanza kuhitimika Mashindano ya Chamazi Rede Cup 2018,wapo Kundi B wakiwa ni wamwisho awana pount ata moja na wamepoteza michezo mitatu,mabao walio fungwa mpaka sasa ni 8. 

Maoni