Lwandamina asema bado anamatumaini ya kurekebisha makosa.

Kocha wa Yanga, George Lwandamina amekubali kuwa kikosi chake hakikucheza vizuri kama walivyotarahia dhidi ya St Louis ya Shelisheli.

Yanga imeshinda kwa bao 1-0 dhidi ya Washelisheli hao katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Lwandamina raia wa Zambia, anaamini wana nafasi ya kurekebisha makosa yao katika machi ya pili wakiwa ugenini na kufanya vizuri.

“Hatukucheza namna tulivyotaka, tumejitahidi lakini bado tuna nafasi ya kujirekebisha na kufanya vizuri,” alisema.

Lwandamina alilazimika kufanya mabadiliko mwishoni mwa kipindi cha pili ili kupata bao baada ya washambuliaji wake wawili, Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa kushindwa kuonyesha cheche ikiwemo kukosa penalti.

Maoni