Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Majaliwa atoa tamko kuhusu kidato cha tano

RAPWI NEWS 
FRIDAY , 16TH FEB , 2018

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa kila kijiji kinakuwa na shule ya msingi yenye madarasa ya awali na kila tarafa iwe na shule ya kidato cha tano na cha sita.Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza katika ziara yake ya siku saba mkoani Mwanza ambapo amewasisitiza walimu wasijiingize katika masuala ya michango bali wajikite na taaluma.

Waziri Mkuu Majaliwa katika siku yake ya kwanza mkoani humo akiongozana na  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,  amezindua madarasa manne ya kidato cha tano katika shule ya sekondari ya Nyehunge wilayani  sengerema huko na kutoa maagizo hayo.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa ameshtukia ubadhirifu katika mradi wa Maji ambao unasimamia na halmashauri mbili za wilaya ya Sengerema na Buchosa ambapo ametoa maagizo kwa TAKUKURU kuweza kuchunguza juu ya mradi huo.

Maoni