MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA YA SIKU NNE MKOANI IRINGA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana ameanza ziara ya siku nne mkoani Iringa ikiwa na lengo la kuhamasisha shughuli mbalimbali za maendeleo na kuzindua mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania – REGROW.

Mara baada ya kuwasili mkoani Iringa , Makamu wa Rais alifungua wodi mpya katika Zahanati ya Kising’a ambapo aliwaomba wananchi wote wajiunge na mfuko wa bima ya Afya ili waweze kunufaika na huduma bora za afya.“niwaombe sana ndugu zangu kila mmoja ahakikishe ana bima ya afya, bima ya afya ndio mkombozi wako, unapopata mavuno yako weka pesa ya bima ya afya”

Makamu wa Rais alitoa pongezi kwa Wananchi hao kwa mwamko wa kuchangia ujenzi na kutoa eneo lakini pia pongezi kwa umoja wa makampuni ya Asas kwa ufadhili wa shilingi za kitanzania milioni 125.Makamu wa Rais alisema Ilani ya CCM inatuagiza kujenga zahanati katika kila kijiji hivyo ujenzi wa Wodi hii katika Zahanati ya Kising’a ni utekelezaji wa maagizo ya Ilani hiyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi waliojitokeza wakati wa ufunguzi wa wodi katika zahanati ya Kising’a mkoani Iringa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya uendeshaji na uzalishaji wa kiwanda cha Ivori Food & Bevarage cha Iringa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Bw. Suhail Esmail Thakore. (Picha na ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya utengenezaji wa viungo katika kampuni ya GBRI inayozalisha bidhaa za mboga mboga zinazojulikana kama Eat Fresh mjini Iringa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyeshwa baadhi ya bidhaa za mboga mboga za Eat Fresh na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya GBRI Bi. Hadija Jabir.


Chanzo: Michuzi Blog

Maoni