MBARAZA UVCCM DAR AANZA UJENZI WA OFISI ZA KISASA ZA UVCCM DAR ES SALAAM.

Katika kuadhimisha miaka 41 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi, na kuunga mkono Kauli Mbiu ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndg. Kheri Denice James ya "Tukutane kazini" Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa kupitia Mkoa wa Dar es salaam Ndg. Gwantwa Alex Mwakijungu ameanzisha kampeni kabambe ya ujenzi wa ofisi za Jumuiya ya Vijana kwa ngazi za Wilaya na kata  za Mkoa wa Dar es salaam kwa madhumuni ya kujenga heshima ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)  kwa Mkoa wa Dar es salaam.

Ujenzi wa ofisi hizo unategemewa kufanyika katika hatua mbili huku hatua ya kwanza ikihusisha ujenzi wa ofisi za wilaya zote za Mkoa wa Dar es salaam na ile ya pili itakayohusisha ujenzi na ukarabati wa ofisi za jumuiya kwa ngazi za kata.

Kampeni hii imeanzia wilaya ya Kigamboni ambapo jengo la ofisi ya wilaya tayari limeanza kujengwa na linatarajiwa kuisha mapema mwezi wa saba na baadae litafuatiwa na lile ya Ubungo na baadae za wilaya zilizobaki.

Majengo hayo ya ofisi ya kisasa kwa ngazi ya wilaya yatakuwa na ofisi mbili za kisasa,mapokezi na kumbi ndogo ya mkutano itakayo kuwa na uwezo wa kubeba hadi watu 36 kwa wakati mmoja.

Ofisi hizo zitajengwa kwa ushirikiano  wa wanachama na wadau mbalimbali wenye mapenzi mema na Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake Ndg. Dkt.John Pombe Magufuli na zitakuwa ndio ngome kuu za Jumuiya ya Vijana katika kutekeleza majukumu na maelekezo ya Chama kwa vijana wa chama hicho.

UVCCM TUKUTANE KAZINI.

Maoni