MBARAZA UVCCM TAIFA AZINDUA KITABU CHA HATUBEBI MABEGI, ANUNUA NAKALA 200.

Na Shaban Rapwi.

Jumapili 18 February 2018.

Uzinduzi huo umefanyika leo Jumapili 18 February 2018 katika ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chamazi.

Uzinduzi huo uliohudhuliwa na viongozi mbalimbali wa ngazi ya Wilaya wakiwemo wajumbe wa kamati ya siasa Wilaya ya Temeke   ulikuwa wa kipekee na wa kuvutia.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Ndg. Gwantwa alisema Mkalipa amevuka asilimia 100 ya uongozi na sasa amefika asilimia 120, anafanya kazi kubwa kuliko vijana wengi.

Pia alisema wanachamazi inabidi kujivunia kuwa na mtu kama Mkalipa kwani ni kijana  mwenye maono makubwa na ya mbali.

"Hongereni sana wanachamazi kwani mmepata Mwenyekiti wa vijana mwenye maono ya mbali, amethubutu kwa kuwa hakuna kiongozi  yoyote wa UVCCM  aliyethubutu kuandika mambo yatakayowafundisha wengine, hongera kwake" alisema Gwantwa

"Mkalipa ni kijana mbunifu, alikuja na kauli mbiu ya hatubebi Mabegi, Mwenyekiti wa Mkoa akaibeba na kuifanya ya Mkoa mzima na sasa mimi pia naibeba na kuwa balozi mzuri kwa kuwa yaliyoandikwa humu yanafundisha sana" alisema Gwantwa

"Kwa kukiunga mkono kitabu hiki nanunua nakala 200 nitakazowapelekea vijana wengine nchi nzima wasome na kuelewa neno hili, kwani ni kitabu kizuri sana na kinafundisha" alisema Gwantwa

Sambamba na hilo Ndg. Gwantwa aliahidi kuleta kadi 2000 kwa UVCCM Kata ya Chamazi ili kuwapa wanachama wa UVCCM wa Kata hiyo.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Chamazi Ndg. Nasri Mkalipa alimshukuru sana Ndg. Gwantwa kwa kuiunga mkono kauli hiyo sambamba na kuwa kiongozi wa mfano kwa kununua nakala 200.

Maoni