MBUNGE: CCM ITAENDELEA KUTAWALA MPAKA YESU ARUDI

Mbunge wa Jimbo la Makete Prof. Norman Sigalla amesema Chama cha Mapinduzi CCM kitaendelea kutawala mpaka Yesu atakaporudi. 

Akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Makete kilichoketi kwa ajili ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM. 

 Mbunge huyo amesema CCM haina mpango wa kuachia madaraka kwa sasa, mpaka hapo Yesu atakaporudi
Amesema wale wanaofikiri kuwa chama hicho kinatawala bahati mbaya, wasahau kwa kuwa kimepania kuendelea kuwaletea mmaendeleo wananchi. 

Pia amesema atagharamia fedha kwa ajili ya kununua Bendera na kadi za kutosha za CCM ili wanachama wanaotaka kujiunga na chama hicho kwenye mmatawi yote ya wilaya ya Makete wasikose kadi. 

Maoni