MECHI YA LIPULI, NDANDA YASOGEZWA MBELE


MCHEZO uliokuwa uchezwe na timu Lipuli dhidi ya Ndanda katika dimba la Samora mkoani Iringa Wasogezwa mbele kwa maandalizi zaidi. 

Bodi ya Ligi (TPLB), imefanya mabadiliko ya mchezo huo namba 153 kati ya timu hizo mbili uliokuwa uchezwe Ijumaa ya Machi 2 mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa leo, imeeleza kuwa sababu za kusogezwa mbele mchezo huo ni kutaka kuipa nafasi na muda zaidi Ndanda FC kusafiri kutoka Mtwara baada ya kumaliza mchezo wao wakiwa wenyeji dhidi ya Mabingwa watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga.

Ambapo sasa umepangwa kuchezwa Jumatano ya Februari 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nangwana Sijaona. Bodi ya Ligi (TPLB) imeamua mchezo huo wa Lipuli na Ndanda sasa umesogezwa mpaka siku ya Jumapili.Mchezo utachezwa kwenye Uwanja ule ule wa Samora mkoani Iringa. 

Ambapo mzunguko uliopita Lipuli alilazwa chali kwa bao 2-1 na Ndanda wakiwa ugenini katika Dimba la Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara. "Kupelekea mbele kwa mchezo huu sisi wachezaji umetupa muda zaidi wa kuendelea kufanya mazoezi,"amesema Beki namba 4 wa kikosi cha Lipuli, Martin Kazira.

Maoni