MILIONI 64/-ZAHITAJIKA WAZEE WOTE MKURANGA WAPATE VITAMBULISHO VYA MATIBABU-ULEGA

SHILINGI milioni 64 zinahitajika ili wazee wote wilayani Mkuranga mkoani Pwani wapatiwe vitambulisho kwaajili ya matibabu.

Hayo yamesemwa jana na Mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega wakati anazungumza na wananchi wa Kijiji cha Kilimahewa Kaskazini wilayani mkuranga.

Amesema mchakato huo umekwishaanza kwa majaribio katika kata tatu ambazo ni Kisiju,Beta na Mkuranga.Ameongeza kuwa majaribio yaliyofanywa yameonesha mafanikio na tayari vitambulisho 300 vimeshatolewa.

Aidha Ulega ameongeza kuwa nchakato huo kwasasa unaendeshwa kwa awamu mbili ambapo kata 13 zitahudumiwa katika awamu ya kwanza na awamu ya pili wanatarajia kuhudumia kata 12.Amesema awamu ya kwanza Sh.milioni 6 zinatarajiwa kutumika bila kutumia mzabuni.

Amezitaja kata zitakazoanza awamu ya kwanza kuwa ni Tambani,Tengelea,Mipeko,Mkuranga,Mwandege,Vikindu,Kimanzichana,Vianzi,Beta,Kisiju,Mbezi,Shungubweni,na Kiparang'anda.

 Wananchi wa kijiji cha Kilimahewa Kaskazini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega.

 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akisalimiana mara baada ya kuwasiri katika kijiji cha  Kimanzichana Kaskazini  leo mkoani Pwani.

Chanzo : Emmanul,Globu ya jamii

Maoni