MKALIPA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO  NA ALIYEKUWA MGOMBEA WA NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI UVCCM TAIFA NDG. RASHID MOHAMMED RASHID

Leo Jumapili 25 February 2018 

Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Chamazi Ndg. Nasri Mkalipa amekutana na kuzungumza na aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti UVCCM Taifa Ndg. Rashid Mohammed Rashid.

Mazungumzo hayo yalifanyika leo katika eneo la GARDEN Mjini Unguja.

Lengo kuu la mazungumzo hayo lilikuwa ni kuangalia  mustakabali mpana wa siasa za Zanzibar hususani kisiwa cha Pemba.

Akizungumza baada ya Mazungumzo hayo Ndg. Rashid M. Rashid alimpongeza sana Ndg. Mkalipa kwa kutunga kitabu kizuri chenye mafundisho makubwa ndani yake na kuwataka vijana wote nchini kuishi kauli ya HATUBEBI MABEGI sambamba na tukutane kazini.

Pia aliwapongeza UVCCM Kata ya Chamazi kwa kuendelea kudumisha Muungano na kuwataka kuja Zanzibar Mara nyingi zaidi.

Pai akizungumza  baada ya Mazungumzo hayo Ndg. Nasri Mkalipa alimshukuru sana Ndg. Rashid M. Rashid kwa ukarimu na upendo aliouonesha kwake na kuwataka vijana kufatilia sana maagizo na kauli anazozitoa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndg. KHERI JAMES kwani ni zenye matokeo chanya kwa mustakabali mpana kwa JUMUIYA YA VIJANA YA CCM.


NUKUU.

"Siku vijana mkijipambanua kwa umoja wenu, Chama kitawapa nafasi, lakini mkijipambanua kwa chuki na uhasama mtabaki wasindikizaji tu wa wengine, nitasema ukweli daima unafiki kwangu mwiko" - KHERI JAMES , Mwenyekiti wa UVCCM Taifa.

Maoni