MKUU WA WILAYA UBUNGO AWAFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU AKWILINA

Juma tatu 19 February 2018.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Kisare Makori amewatembelea na kuwapa pole familia ya marehemu Akwilina Akwilini.

Mheshimiwa Kisare Makori aliitembelea familia hiyo ya marehemu inayoishi Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam leo Jumatatu 19 February 2018.

Marehemu Akwilina alipatwa na umauti baada ya kupigwa risasi ya kichwa katika eneo la Kinondoni Mkwajuni siku ya tarehe 16 February 2018.

Kabla ya kupatwa na umauti Marehemu Akwilina  alikuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo cha usafirishaji (NIT).

Mkuu wa Wilaya aliongoza na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg. John Lipesi Kayombo na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg. James Mkumbo.

Poleni sana ndugu, jamaa na marafiki wa Akwilina.

Bwana ametoa, bwana ametwaa.

Jina lake lihimidiwe.

Picha zote na
Kitengo cha Habari na Uhusiano 
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo 

Maoni