Msufini yaicharaza Saku bao 4-0 Uvccm Chamazi Rede Cup 2018.

Msufini leo imeiendesha mchakamchaka Saku kwa kuigonga kipigo kizito cha mabao 4-0 kwenye mchezo wa michuano ya Uvccm Chamazi Rede Cup.

Aina ya ushindi iliyoupata Msufini na kasi iliyoonyesha mchezoni,ilitosha kabisa kwa mashabiki kuifananisha timu hiyo na ile kasi ya juu ya mtandao wa 'Intanet' ya 4G.

Ushindi huo mnono unaifanya Msufini kuwa miongoni mwa team bora kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo ikiwa kileleni mwa Kundi B baada ya kufikisha point tisa.

Ushindio huo umeiongezea rekodi Msufini katika mechi za mashindano ya Uvccm Chamazi Rede Cup ambapo hivi sasa rekodi inasomeka kuwa katika mechi 3 walizo cheza,imeshinda zote na wamefunga mabao 10.

Maoni