MSUFINI YAWEKA REKODI UVCCM CHAMAZI REDE CUP 2018.

Na Shabani Rapwi, Chamazi

Timu ya Msufini imeweka rekodi kuwa timu pekee kumaliza mzunguko wa kwanza katika mashindano ya UVCCM CHAMAZI REDE CUP 2018 bila kuruhusu kufungwa hata bao moja.

Msufini wamemaliza mzunguko wa kwanza kwa kuifunga timu ya Mzambarauni bao 1-0.

Msufini walianza mchezo wao wa kwanza kwa kuifunga Kwa Mkongo bao 4-0 ,wakaifunga Dovya B 2-0 kisha kuifunga Saku kipigo kitakatifu cha  mabao 4-0 na kuifunga Dovya A 5-0

Msufini inaongoza Kundi B ikiwa na point 15 na mabao 16.

Maoni