MUWSA MABINGWA UTOAJI HUDUMA BORA ZA MAJI TANZANIA

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji,Aisack Kamwelwe ameiagiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) kuukagua mradi wa maji wa Buchosa uliopo Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza kwani anazotaarifa kuna vifaa vimenunuliwa havina ubora kabisa.

Maagizo hayo aliyatoa jana Mjini hapa wakati akizindua ripoti na utendaji wa Mamlaka za Maji za Miji na Mikoa na miradi ya kitaifa.

Uzinduzi huo uliandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ambapo Mamlaka ya Maji ya Moshi ilichaguliwa kuwa ya kwanza kwa utoaji bora wa huduma za maji. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe (kulia) akimkabidhi tuzo ya ushindi wa Mamlaka inayotoa huduma bora za Maji Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi (MUWSA) ,Prof. Faustine Bee. Kushoto ni Mkurugenzi Mkurugenzi Mkuu wa MUWSA, Joyce Msiru. Makabidhiano hayo yalifanyika mjini Dodoma juzi.

Maoni