NAIBU WAZIRI MADINI ATUA MKOANI SONGWE KWA ZIARA YA KIKAZI

Na Mathias Canal, Songwe

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko leo 22 Februari 2018 ameanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Songwe ambapo pamoja na mambo mengine atatembelea na kukagua eneo la mgodi tarajiwa wa Bafex linalotarajiwa kuanza uchimbaji wa Madini ya dhahabu.

Maeneo mengine atakayotembelea ni pamoja na mgodi wa uchimbaji dhahabu wa Shanta Gold Mine uliopo katika kata ya Saza, Wilayani Songwe ambapo atazungumza pia na wafanyakazi wa mgodi huo.

Sambamba na hayo pia Naibu Waziri wa Madini atazungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano ulioandaliwa Mara baada ya kutembelea maeneo ya uchimbaji.

Mara baada ya kuwasili katika Mkoa wa Songwe Mhe Biteko amesifu juhudi za mbunge wa Jimbo la Songwe Mhe Philiph Mulugo kutokana na uwajibikaji mkubwa katika kuwasemea wananchi wa jimbo hilo hususani katika kuimarisha uchumi wa wananchi kupitia sekta ya Madini.

Naibu Waziri wa Madini, Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza mara baada ya kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Songwe kwa ajili ya ziara ya siku mbili ya kikazi katika mkoa wa Songwe, Leo 22 Februari 2018.

Naibu Waziri wa Madini, Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Songwe, na Kamati ya  siasa ya CCM Wilaya hiyo mara baada ya kuwasili Mkoani Songwe kwa ziara ya kikazi, Leo 22 Februari 2018.

Mkuu wa wilaya ya Songwe, Mhe Samwel Jeremiah akieleza changamoto za wachimbaji wadogo katika Wilaya hiyo mbele ya Naibu Waziri wa Madini, Mhe Doto Mashaka Biteko wakati akisoma taarifa ya Mkoa wa Songwe kwa niaba ya mkuu wa Mkoa huo, Mhe Chiku Galawa, Leo 22 Februari 2018.

Maoni