Ndege ya jeshi la Israel yaanguka.

Ndege aina ya F16 ya jeshi la Israel imeanguka baada ya kushambulia ngome za Iran zinazopatikana nchini Syria.

Jeshi la Israel  limefahamisha kuwa linafuatilia kwa karibu  tukio hilo na kusema kuwa lipo tayari kwa operessheni muda wowote.

Seriakli ya Assad amefahamisha kuwa jeshi la Israel la anga  limeendelea kushambulia Syria baada ya ndege yake ya F16 kuanguka.

SANA shirika la habari la Syria limefahamisha kuwa ndege za kivita za Israel limeshambulia ngome  za Iran mapema Asubuhi Jumamosi.

Tangazo lingine limefahamisha kuwa  mashambulizi ya Israel Syria yaliendelea kwa muda kadhaa.

Serikali ya Israel imetangaza kufungwa anga la Tel Aviv kwa safari zote za ndege.

Maoni