Rais Magufuli amteua Meja Jenerali Yakubu Hassan kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ.

Download and play musics

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 14 Februari, 2018 amemteua Meja Jenerali Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Pamoja na uteuzi huo, Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo kutoka Meja Jenerali na kuwa Luteni Jenerali.

Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed anachukua nafasi ya Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa ambaye amestaafu.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapandisha vyeo kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali wafuatao;

    Brig Jen. J.G. Kingu 

   Brig Jen. M.S. Busungu 

   Brig Jen. R.R. Mrangira  

  Brig Jen. B.K. Masanja 

   Brig Jen. G.T. Msongole 

   Brig Jen. A.F. Kapinga

    Brig Jen. K.P. Njelekela 

   Brig Jen. A.S. Bahati  

  Brig Jen. M.E. Mkingule 

   Brig Jen. S.S. Makona

Mabrigedia Jenerali wote waliopandishwa vyeo watapangiwa vituo vya kazi baadaye.

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed ataapishwa kesho tarehe 15 Februari, 2018 saa 5:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

14 Februari, 2018.

Maoni