SAID P,ATIMIZA AHADI YAKE

Na shabani rapwi. 

Katibu wa diwani kata ya chamazi  Ndg. Said Paul (Said P) ametimiza ahadi yake aliye itoa wiki mbili zilizo pita,yakutoa mipira miwili kwa team ya Mbande Magengeni inayo shiriki mashindano ya Uvccm chamazi rede cup 2018.

Akizungumza wakati wa ukabidhi wa mipira hiyo hapo jana Ndg. Said P alisema

 " Zoezi ili ni endelevu kwa kila team zinazo shiriki mashindano haya ya Uvccm chama rede cup 2018  lengo  langu kubwa ni kuunga mkono mashindano haya ya rede na michezo kwa ujumla na pia kumuunga mkono Mh Hemedi Juma Karata Diwani wa kata yetu ya Chamazi kwa utekelezaji mzuri"

Pia Said P aliwaomba na kuwataki viongozi kuwa na ushirikiano, kuanzia ngazi ya Kata mpaka kwenye matawi kwani ndio Msingi wa maendeleo. 
(Pichani ni Katibu Hamasa na Chipukizi tawi la Mbande Magengeni) 

Kwa upande wake Katibu Hamasa na Chipukizi tawi la Mbande Magengeni Ndg. Mohammed Omary Mohammed (Adedi) amemshukuru Said P na kuwataka viongozi wengine kuiga mfano wake.

"Tunakushukuru sana kiongozi wetu kwa kutusaidia maana tulikuwa tunapata shida sana kwenye swala la mipira rakini sasa ukata wa mipira umekwisha,kama viongozi wote wange kuwa wanajitolea ivi timu nyingi zisingekuwa na changamoto nyingi sana" alisema Adedi

Adedi alizungumzia namna walivyo jipanga kwa raund ya pili ya mashindano ya Uvccma chamazi rede cup 2018.

"Tumejipanga vizuri kwa raund ya pili kufanya maajabu jambo raund ya kwanza tumejitaidi kwa upande furani, tumepoteza mechi tatu na kushinda mechi mbili, sasa kwa raund ya pili tunataka tushinde zote" alisema Adedi. 

Maoni