SHEIKH MKUU MKOA WA DAR: MWISHO WA MANGE MITANDAONI UMEFIKA.

 
Al Haji Mussa Salimu ambae ni Sheikh mkuu, mkoa wa Dar es Salaam ametahadharisha kuwa huu ndo mwaka wa mwisho kwa mwanadada maarufu mitandaoni, Mange Kimambi kutumia mdomo wake kuwatukana watu hasa Viongozi.

Akiongea na wanahabari leo Jumatatu Februai 5 2018, amesema kuwa anasikitishwa sana picha zilizopigwa siku ya mazishi ya Sheikh Masoud zinatumika vibaya mitandaoni na mwanadada huyo anayemsadiki kutumika.
Amesema wanatumia utaratibu wa kisheria kuwadhibiti wote wanaoandika habari ambazo hazina ukweli huku akiwatuhumu Gazeti la Tanzania Daima kwa chapisho la leo lenye kichwa cha habar, SHEIKH ACHAFUA HALI YA HEWA na baadhi ya vyanzo vingne nchini.

“Tutafanya utaratibu wa kisheria kwa wale wote walioingia kichwakichwa kuandika habari ambazo hazima ukweli wakiwamo Jamii forum na magazeti ya Tanzania Daima, nataka wanionyeshe ukweli wa hiyo taarifa”. Amesema Al Haji Mussa.

Ameongeza kwa msisitizo kuwa wote wanaotafuta umaarufu kupitia midomo kwa maneno machafu huku akimtaja Mange Kimambi, wacheze na watu wengne na sio viongozi wa dini.
“Tunamwambia huyo anayejiita Mange kimambi acheze na watu wengine na sio viongozi wa dini, huu ndio mwaka wa mwisho kwake tutasema na Mwenyezi Mungu na majibu mtayaona”. Amesema Al Haji.

Chanzo : Darmpya

Maoni