TV zilizofungiwa zarejea hewani

Kwa ufupi
Vituo vya televisheni vilivyofunguliwa ni NTV na KTN News, na ambavyo havijafunguliwa ni Citizen TV na Inooro TV.
Vituo hivyo vilifungwa na Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) Januari 30 baada ya kukaidi agizo la kutaka visirushe matangazo mbashara kuhusu kuapishwa kwa kiongozi wa muungano wa Nasa, Raila Odinga kuwa rais wa watu.

by Taboola
Habari MONDAY, FEBRUARY 5, 2018
TV zilizofungiwa zarejea hewani
 0    
     
   
Nairobi, Kenya. Vituo viwili vya televisheni kati ya vinne ambavyo vilikuwa vimefungwa na serikali siku saba zilizopita vimefunguliwa.
Vituo vya televisheni vilivyofunguliwa ni NTV na KTN News, na ambavyo havijafunguliwa ni Citizen TV na Inooro TV.
Vituo hivyo vilifungwa na Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) Januari 30 baada ya kukaidi agizo la kutaka visirushe matangazo mbashara kuhusu kuapishwa kwa kiongozi wa muungano wa Nasa, Raila Odinga kuwa rais wa watu.
Televisheni ya NTV inayomilikiwa na kampuni ya Nation Media Group ndiyo ilikuwa ya kwanza matangazo yake kusitishwa ikafuatiwa na Citizen TV inayomilikiwa na kampuni ya Royal Media Services Ltd.
Saa mbili baadaye, KTN inayomilikiwa na Standard Group ilizimiwa matangazo yake.
Hatua ya kufungwa matangazo ya televisheni hizo ilishutumiwa na Umoja wa Mataifa, Marekani, Umoja wa Ulaya na mashirika ya haki za binadamu.
Vyombo vya habari vya kimataifa vimeangazia hatua ya serikali kukaidi kutii amri ya mahakama iliyotaka matangazo ya televisheni hizo yafunguliwe.

Chanzo : Mwananch

Maoni