ULIPO UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM NIPO - MKALIPA

Mwenyekiti wa Uvccm Kata ya Chamazi, Ndg Nasri Mkalipa kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook mkalipa ameandika popote palipo na utekelezaji wa ilani ya CCM na yeye yupo.

Ameyandika hayo baada ya kupata mwaliko toka kwa Diwani wa Kijichi Mh Mtarawanje hapo Jumamosi na kushiriki zoezi la usafi.

Post ya mkalipa ilikuwa inasomeka ivi 

"ULIPO UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM NIPO (picha iko chini)  Hapa ni Kata ya Kijichi baada ya kupata mwaliko katika zoezi LA usafi lililoandaliwa na Diwani wa Kata hiyo Mh. MTARAWANJE.
Zoezi hilo lilifanyika siku ya JUMAMOSI 10 February  2018.
Sikwenda peke yangu, niliongozana na viongozi wa ngazi ya Kata na Matawi sambamba na baadhi ya wanachama takribani 30 kutoka Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chamazi.
Yote ni katika kuendelea kujifunza na kutoa sapoti kwa Kata zingine.
UMOJA, UPENDO NA MSHIKAMANO NDIO SILAHA YETU.
# DSM HatubebiMabegi.
# TukutaneKazini"

Maoni