UMOJA WA VIJANA WA CCM (W) NZEGA

Tarehe 21/2/2018 ni ziara ya siku ya pili tangu Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Nzega ndg. Nzuki Machibya Sengelema kuanza ziara yake ya kiwilaya ambapo alitembelea Kata mbili ya MIGUWA na MBOGWE.

Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Nzega ndg. Ibrahim Kijanga kabla ya kumkabidhi Mwenyekiti kuongea na vijana baada ya utambulisho wa viongozi wote alianza kwa kusisitiza viongozi waanze sasa kufanya vikao vyao vya kikatiba na vizingatiwe bila kupuuzwa kwani huo ndio msingi wa kwanza wa viongozi kwa wanachama na viongozi wa CCM.

"Viongozi lazima muwaandae vijana kimaadili ktk masuala ya uongozi kwa mjibu wa katiba ya CCM.
Ili vijana kweli waweze kuwa viongozi wazuri wa baadaye lazima wapikwe ktk tanuri kupitia Jumuiya hii ya vijana, Katibu uenezi wa CCM hili ni jukumu lako kuwafunda vijana".

"Naomba mtambue kuwa CCM MPYA si ile ya mazoea ya kuwekana wekana kwenye nafasi za uongozi kisha mnasubiri kipindi cha uchaguzi tu, ikiwa kuna viongozi wa namna hiyo ni bora muanza kuwaondoa mara moja kwa mjibu wa katiba na kanuni zinavyowaongoza.
Mimi kama Katibu sitakubali uzembe huu, kama tatizo ni uongozi wa chama ktk matawi basi ipo haja nyinyi viongozi wa Kata - ya kuchukua hatua dhidi yao, vijana hawawezi kujua wanaelekea wapi iwapo uongozi wa tawi haukai vikao vyake wala kuwaelekeza cha kufanya".

"Hii ni ziara ya Mwenyekiti sitatumia muda mwingi kuzungumza, lakini nitakuja mwenyewe kwa mara nyingine tubanane na yeyote atakayekwamisha maagizo haya nayoyatoa hapa.
Nimalize kwa kumuomba mwenyekiti Kata amkaribishe Mwenyekiti ili azungumze na vijana".

Aliyoyasema Mwenyekiti baada ya kukaribishwa kuongea na vijana.....

"Ndugu zangu, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zote kwa ujumla pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi.
Jambo la kwanza sina budi kuwashukuru vijana wenzangu kwa kuniamini na kunipa jukumu hili kuwaongoza, nawashukuru sana, mlinikopesha kura zenu, na sasa ni wakati wangu wa kulipa deni hilo.
Mimi nawalipa maendeleo yenu na kwa kuimarisha wa Jumuiya hii.
Nataka vijana kuhakikisha mnajikwamua  kiuchumi ktk nyanja mbalimbali kupitia fursa zilizopo ktk Wilaya yetu ya Nzega.
Ili vijana muweze kushiriki kazi za chama CCM lazima kwanza muutawale uchumi wenu, unapoutawala uchumi hutakubali kununuliwa na mtu kifikra na kiuchumi, haya yanaweza kuondoka iwapo vijana mtaondokana na mazoea ya kutegemea msaada watu wababaishaji wala rushwa za viongozi wasio wema na wanaojitokeza wakati wa uchaguzi.
Nimefika hapa ktk Kata yenu ya Mbogwe lakini vijana wengi naambiwa wamekwenda kulinda  mpunga  usishambuliwe na ndege, napata wakati mgumu kuamini moja kwa moja hoja hii kwa sababu vijana nawajuwa hamuishi vijasababu na mzaha ktk mambo ya msingi.
     Leo hii ni siku ya ziara ya Mwenyekiti wenu wa Wilaya nimekuja, na hii ni ya mara moja baada muda fulani, imekuwaje wazazi waje hapa ktk kikao kwa niaba ya vijana wakati kikao hiki ni cha vijana?
Na kikao hichi kinaweza kuchukua masaa mawili tu kinakwisha, ni kwa nini sasa wazazi wasigewashikia huko wanakolinda ndege haya masaa mawili tukaelezana masuala ya msingi kwa chama chetu na kwa maendeleo yao vijana kiuchumi ambapo faida yake inamgusa moja kwa moja mzazi?
Kitendo hichi kimeninyong'onyesha sana kukuta vijana hapa ni wachache.
Sasa hivi serikali yetu ya chini ya Rais John Pombe Magufuli imekuja na majibu ya changamoto za vijana kuhusu ajira, imetenga fedha za kutosha za vijana ktk kila Halmshauri za Wilaya ili vijana wakopeshwe na wajiajiri wenyewe.
Tena mkopo wenye masharti nafuu kabisa, lakini vijana hamjitokezi kuhiriki hili.

Yaani vijana mnasubiri Uchaguzi Mkuu ufike ili muungane na wapotoshaji wanaopotosha mitandaoni na ktk mikutano ya kisiasa kwamba "serikali ya CCM imeshindwa kusaidia vijana kwa kutowaajiri au kukopesha" mikopo?.
Sasa hivi fedha zipo ktk Halmashari yetu mnangoja nini kukopa na kujiendeleza ktk kazi mnazotaka kuzifanya?
Ndoto yenu kimaendeleo ikoje sasa ikiwa serikali imewaletea fedha zenyemasharti nafuu?.

Nawashangaa sana, tumeamua kufanya kambi la ujasiriamali naomba wazazi muwape ruhusa vijana ili vijana wapewe elimu ya ujasiriamali huenda itawasaidia vijana kujitambua zaidi."

"Nchi yetu kitakwimu, asilimia 28 ya watanzania ni masikini, na asilimia  75 wengi wao wako vijijini na ndiyo wakulima ambao wako huku vijijini.
Nikitolea mfano wa nchi zilizoendelea, nchi ya Marekani asilimia kubwa ya matajiri wa Marekani ni wakulima, lakini cha ajabu Tanzania hao wakulima kwa nchi yetu ni masikini wa kutisha, hii ni aibu.
Chama hiki (CCM) ni cha Wakulima na Wafanyakazi, na chama hiki ndicho kinachoongoza nchi, nasema hivi! haiwezekani kuwaona wakulima mnaachwa nyuma kimaendeleo, lazima tushiriki maendeleo kwa vitendo.
Nimeongea na Waziri wa Kilimo ndg. Kizeba na aliniahidi kuniunga mkono kupitia Kilimo ktk Wilaya yetu, kwa hiyo vijana changamoto zinazowahusu kupitia kilimo Waziri ameahidi kutuunga mkono".

WAZEE WAMTABIRIA MAKUBWA:

Wakizungumza ktk kikao hicho, viongozi wastaafu wa Kata ya MIGUWA, wazee waliohudhuria ktk mkutano huo wamemtabiria makubwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Nzega ndg. Sengelema wakisema    "   ....Kijana unajitahidi sana kuongea maneno mengine mazito, lakini hatujui kama mtaweza kumfikia NYERERE, labda MAGUFULI, sisi wazee wako tunakuombea ukivuka hapa ulipo Mungu akupe kiti (ngazi nyingine) kingine cha kuwatumikia watu.
Nimekusikiliza kwa makini sana, umeongea vizuri sana, ikiwa viongozi mtakuwa hivi wote, basi ile kiu yetu kuhusu changamoto za vijana zitakwisha.
Mungu akutangulie kijana".

Mwenyekiti Sengelema aliwashukuru wazee kwa maoni na ushauri wao.
"Wazee wangu nawashukuru kwa maoni na hekima zenu, nimewasikia na nitayatii maneno yenu, lakini mengi tumwachie Mwenyezi Mungu kwani yeye pekee ndiye mwenye mamlaka zaidi.
Nitatumikia vijana wenzangu kwa kadiri niwezavyo.....

La mwisho nakumbusha kuwa, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Tabora alikuja ktk Wilaya yetu ya Nzega na kutoa maagizo kwamba vijana mlete cv zenu ili muweze kutafutiwa nafasi za ajira kutokana na kwamba serikali kupitia wizara mbalimbali ina mahitaji ya waajiriwa kupitia wizara na mashirika ya umma yaliyopo.
Viongozi wa vijana leteeni cv zenu kwa viongozi wataziwakirisha kwetu.

Naomba niwatakie majukumu mema, lakini kumbukeni yale yote tuliyoyasisitaza yafanyike bila mizengwe, natambua kuwa mmenichagua niwatumikie, sasa sitaweza kumvulia kiongozi mzembe ktk uongozi wangu.
Asanteni"

Imetolewa na Idara ya Habari na Uhamasishaji UVCCM Wilaya ya Nzenga.

Kwiyeya Singu

Maoni