UVCCM CHAMAZI YAANZA TOUR YA HATUBEBI MABEGI ZANZIBAR.

Ijumaa 23 February 2018.

Dar - Zanzibar

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chamazi umeanza rasmi ziara yake ya kutembelea Mikoa mbalimbali kwa ajili ya uzinduzi wa Kitabu kilichojipatia umaarufu cha HATUBEBI MABEGI ambapo leo watakuwa Zanzibar  mpaka 26 February 2018.

Katika ziara hiyo UVCCM Kata ya Chamazi imewakilishwa na Mwenyekiti wake NASRI MKALIPA, Katibu JUMA BEGA ZONZO, Katibu Hamasa na Chipukizi NAJIM NYANZA na Mkuu wa Idara ya Burudani na Michezo Ndg. MUHUNZI ALLY MUHUNZI.

Kitabu hicho kizuri kinachotia ujasiri kwa vijana kilizinduliwa rasmi Mkoa wa Dar es Salaam na Mjumbe wa baraza Kuu UVCCM Taifa Ndg. GWANTWA ALEX MWAKIJUNGU.

Katika ziara hiyo itakayochukua siku tatu, sambamba na uzinduzi wa Kitabu cha HATUBEBI MABEGI, UVCCM Kata ya Chamazi itatembelea maeneo mbalimbali ya Zanzibar.

Akizungumza kabla ya kuanza safari hiyo Katibu wa UVCCM Kata ya Chamazi Ndg. JUMA BEGA ZONZO alisema ni bahati iliyoje Kata ya Chamazi kuaminiwa na viongozi wakubwa wa UVCCM na kupewa nafasi ya kutembelea mikoa mbalimbali ya Tanzania.

"Tunamshukuru Mungu Kata yetu inaaminika sana yote haya hayakuja kimiujiza ni kwa sababu ya kufanya kazi" alisema Bega.

"Nasisi tutakuwa mabalozi na waalimu wazuri wakuwalekeza wenzetu jinsi gani wafanye na wao wawe bora na kuweza kutekeleza ilani ya CCM" alisema Bega.

"Tutakuwa mabalozi wazuri wakuwaelekeze viongozi wa Vijana wa Kata zote nchini kuwa unaweza kufanya mambo makubwa bila kujali nafasi yako na watu wakakuamini" alisema Bega.

SHUKRANI ZETU ZA PEKEE

Shukrani zetu za kipekee ziwafikie viongozi wakuu wa UVCCM Taifa chini ya Mwenyekiti KHERI JAMES kwa kuwa wawazi na kututia moyo pale tunapofanya vizuri, kwani imekuwa ni chachu ya sisi kufikiria mambo mapya yatakayofanya Chama Cha Mapinduzi kuendelea kuaminika nchi nzima.

Pia Mwenyekiti wetu wa UVCCM Mkoa wa Dar as Salaam Ndg. MUSSA KILAKALA kwa kutulea vyema na kutupa mawazo chanya kila kukicha.

Bila kumsahau Mshauri Mkuu wa Mwenyekiti wa UVCCM Chamazi Ndg. NASRI MKALIPA, Mshauri huyo ni Katibu wa UVCCM Wilaya ya Ubungo Ndg. LEAH D. MBEKE kwa hakika umekuwa ni mshauri bora.

Pia zimfikie Katibu wa UVCCM Mkoa wa Kusini Unguza Ndg. ALAWI HAIDAR FOUM kwa maandalizi mazuri ya uzinduzi huo sambamba na kuwandalia maradhi na makazi kwa muda wote wa siku tatu.

Mungu ambariki sana.

#DSM HatubebiMabegi.

#TukutaneKazini.

Imetolewa na

Idara ya Hamasa na Chipukizi

UVCCM Kata ya Chamazi
Picha zote na Katibu Hamasa na Chipukizi kata ya chamazi Ndg Najim Nyanza. 

Maoni