UVCCM MKOA WA KUSINI NA UVCCM KATA YA CHAMAZI NI NDUGU WENYE UMOJA WA KUHAKIKISHA CHAMA CHA MAPINDUZI KINAZIDI KUIMARIKA NA KUBAKI MADARAKANI DAIMA.

Umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Kusini na UVCCM Kata ya Chamazi ni ndugu wenye umoja wa kuhakikisha chama cha Mapinduzi kinazidi kuimarika na kubaki madarakani daima.

Viongozi UVCCM kata ya Chamazi leo Fabruari 23 na kesho Fabruari 24 wako Zanzibar Mkoa wa Kusini Unguja kwa lengo la kuimairisha chama leo baada ya mapokezi walipelekwa Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ziara ya kazi za kuimarisha chama na kukaguwa utekelezaji wa ilani. 

Wageni hao kutoka Chamazi wenyeji wa Mkoa wa Kusini leo walikwenda Kaskazini Unguja kwa lengo lile lile la kuimarisha chama kwa maana Mikoa yote ya znz inafanya kazi kwa pamoja na mashirikiano.

Walivyokuwa kuwa Mkoa wa Kaskazini walitembelea kiwanda cha sukari Mahonda walipachika bendera mpya na kushusha chakavu kwa mabalozi hatimie walifika Nungwi kuangalia mradi wa ufugaji samaki na kasa. 

Kesho Fabruari 24 Mkoa wa Kusini Unguja kutakuwa na semina elekezi kwa wajumbe wa kamati za utekelezaji Majimbo yote ya Mkoa wa Kusini Wilaya zote na Mkoa.

Semina hiyo elekezi ni kwa ajili ya mafunzo maalum ya kazi kwa viongozi wapya na Mgeni rasmin atakaefunguwa semina hiyo ni Mh Ramadhani Kichupa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja.


Ugeni huo kutoka kata ya Chamanzi unaongozwa na Mwenyekiti wa kata hiyo Nd Nassir Bakar ameongoza na Katibu kata ya Chamanzi katibu hamasa na mratibu wa michezo kata hiyo.

Maoni