WANACHAMA 500 UVCCM KUPEWA KADI LEO CHAMAZI

(Picha hii ni mfano wa Kadi rakini haiusiani na tukio la leo) 

Leo Jumatano Februari 14, 2018.

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM kata ya Chamazi, Leo unatarajia kutoa kadi kwa Wanachama Wapya zaidi ya 500,zoezi ambalo litafanywa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Wilaya ya Temeke Ndg. Fadhil Mohammed (FAMONGA) kwenye ofisi ya Tawi la CCM Kisewe hii leo.

Mgeni rasmi katika sherehe hizo anatarajiwa kuwa Mstahiki Meya wa Mansipaa ya Temeke Mh. Abdallah Chaurembo.

Pia kwenye sherehe hizo zitaambatana na mchezo mkali wa Mpira wa Miguu kati ya mashabiki wa Simba Sc na Yanga Sc.
 

Maoni