WAPIGA DILI,WALA RUSHWA HAWATAKIWI CCM

MWENYENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya kiwalani Mathias Kahinga Amesema katika kipindicho chote cha uongozi wake wapigaji, wala rushwa, pamoja na wapiga dili hawana nafasi kwenye utawala wake nakudai mbeleko za kuwabebea zimechanika.

Amesema kwake ni kuchapa kazi aliyotumwa na wanachama wa Chama chake kwa lengo kuu la kutatua na kuisimamia Serikali huku akitoa rai kwa viongozi wezake ndani ya chama hicho kuhakikisha wanakuwa waadilifu na wenye unyenyekevu kwa wananchi na kutatua kero zao.

Mwenyekiti na kada huyo wa Chama ameyasema haya jijini Dar es salaam katika ofisi za Chama hicho Kata zilizopo Kata hiyo ya kiwalani ndani ya manispaa ya Ilalat. Ambapo amesema kwake wapiga dili na wezi hawana nafasi kabisa.

"Nilikuwa na mambo kadhaa ambayo nilihaidi kwa wanaccm wakati nautaka uwenyekiti na moja ya kazi yangu kubwa ni kurejesha mtaa mmoja wa serikali ya mtaa ambao unatawaliwa na CUF kwa miaka 15 sasa na hakuna maendeleo yeyote ndani ya mtaa huo wa kigilagila. "amesema Kahinga

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kata ya Kiwalani,Mathias Kahinga kulia)akizungumza na waaandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya wapigaji, wala rushwa, pamoja na wapiga dili hawana nafasi kwenye utawala wake, jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Chama hicho Kata kiwalani,Eva Malenga (kushoto) akisisitiza jambo katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

Maoni