WASOMI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) WAKIFURAHIA KITABU CHA HATUBEBI MABEGI

Jumapili 25 February 2018.

Leo Jumapili Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chamazi Ndg. Nasri Mkalipa amekutana na kuzungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Tawi la Mabibo Hostel.

Tawi hilo linaongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Ndg. Isack Naftar Ngombe na Katibu Ndg. Chacha Malima.

Katika mazungumzo hayo Ndg. Mkalipa alielezea mada juu ya kauli mbiu ya Mkoa wa Dar es Salaam ya hatubebi Mabegi sambamba na mustakabali mzima wa siasa za taifa letu.


Akizungumza kwa niaba ya wanachama wa Tawi hilo Mwenyekiti wa UVCCM wa Tawi hilo Ndg. Isack Naftar Ngombe alisema amefurahi sana kuona Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tukitembelea sambamba na kupeana elimu juu ya mambo mbalimbali.

Pia alimpongeza Ndg. Mkalipa kwa uthubutu wa kuandika kitabu chenye kuleta tija kwa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi.

"Nakupongeze Ndg. Mkalipa kwa kuandika kitabu kizuri ambacho kinatutaka sisi vijana kuishi katika misingi ya Chama na sio kuwa Vijana wa hovyo" alisema Ndg. Ngombe

"Umeeleza vizuri maana ya neno Hatubebi Mabegi sambamba na Tukutane kazini nasisi tumeelewa na tunaahidi kuwa mabalozi wazuri huko tunapoenda kipindi cha likizo" alisema Ngombe

NUKUU.

"Tunataka kuona katika taifa hili, Vijana jeuri na wenye kujiamini, si Vijana waoga akina ndio bwana mkubwa, vijana wanaohoji na kupiga Vita mifumo ya jamii isiyoshabihiana na matakwa na matarajio ya jamii ya Kitanzania, tunataka vijana waasi dhidi ya  mifumo kandamizi, ubwana na ufisadi katika taifa"

Maoni