WATU 17 WAMEUWAWA

Watu 17 wameuwawa kufuatia risasi zilizofyetuliwa na kijana wa miaka 19 katika shule moja huko Parkland katika jimbo la Marekani la Florida. Duru za hospitali zinasema wengine 14 wanatibiwa, watatu kati yao hali yao ni mahtuti.

Aliyefanya shambulio hilo amekamatwa.

Polisi wanasema kijana huyo alifukuzwa katika shule hiyo kwa makosa ya ukosefu wa nidhamu.

Kwa mujibu wa seneta Bill Nelson, kiijana huyo alibonyeza kengele ya kutoa tahadhari ili kuwavutia wanafunzi watoke nje.

Wanafunzi wenzake wanamueleza kuwa kijana mpweke anayependa kuchezea silaha na visu.

Chanzo : Dw Kiswahili

Maoni