YALIYOSEMWA KAMPENI ZA CCM KUMNADI MGOMBEA UBUNGE (CCM) KINONDONI MHE. MTULIA KATA YA KIGOGO TAR. 12FEB



"Nawakumbusha Maulid Mtulia alitoa pesa za usafishaji wa mifereji kutoka mfuko wa jimbo" - John Manyama, Diwani Kata ya Kigogo

"Mtulia alishirikiana na Naibu Meya Ilala, John Manyama kutafuta pesa za kujenga zahanati kata ya Kigogo" - John Manyama, Diwani Kata ya Kigogo

"Ni Mtulia huyu huyu alishirikiana na Diwani wa Kigogo kutafuta pesa za maboresho ya masoko" - John Manyama, Diwani Kata ya Kigogo

"Ukimchagua Mtulia kwa kura ya ndiyo, njia ya kuyafikisha matatizo yenu kwa mamlaka husika yapatiwe ufumbuzi ni nyeupe" - Mama Salma Kikwete (MB)

"Mchagueni Mtulia kwa sababu ametulia kunadi sera, ilani ya uchaguzi na ana uwezo wa kutekeleza kwa vitendo" - Juma Aweso, MB (Pangani)

"Chadema haina uwezo ya kuwaletea maendeleo. Mchagueni Mtulia akashirikiane na Serikali ya Rais Magufuli kuwaletea maendeleo" - King Msukuma, MB

"Mtu akitoka CCM na kwenda upinzani hajanunuliwa, ila akitoka upinzani kwenda CCM amenunuliwa. Kununuliwa ni hoja nyepesi ya Watu walioshindwa tayari." - Hussein Bashe, MB (Nzega Mjini)

"Sisi tuliokuja kumuombea kura Mtulia, tutahakikisha Mtulia akishinda ana simamia haki zenu" - Hussein Bashe, MB (Nzega Mjini)

"Kilio cha Watu wa Kigogo na Watu wa Kinondoni ni vilio vyetu sote. Tutashirikiana na Mtulia kuhakikisha tunamaliza shida, karaha na matatizo yenu" - Hussein Bashe, MB (Nzega Mjini)

"Mchague Mtulia kwa sababu anatoka kwenye Chama Cha Mapinduzi kinachoongoza dola na chenye ilani ya uchaguzi" - Mtulia

"Nichagueni kwa sababu ni sehemu yenu, ninayajua matatizo yenu. Nipo tayari kuyatatua kwa sababu nipo kwenye timu imara yenye dola na yenye ilani inayoongoza nchi" - Mtulia

"Mtulia huyu huyu ndio yule yule alizuia bomoabomoa kwa wakazi wa Mabondeni wakiwemo wakazi wa Kata ya Kigogo" - Mtulia

"Mkimchagua Mtu mwingine ambaye hana mahusiano mema na Serikali, anaituka Serikali kila siku msitegemee kuletewa maendeleo kwa mazingira hayo" - Mtulia

"Nichagueni nikahakikishe Marehemu waliokufa wakiwa na madeni, wanasamehewa na Serikali." - Mtulia

"Mkinichagua nitashirikiana na Meya kuhakikisha tunabadili mfumo wa taa za barabara kutoka kutumia umeme wa Tanesco mpaka kutumia umeme wa jua" - Mtulia

"Mkinichagua nitahakikisha Polisi hawawasumbui tena waendesha bodaboda." - Mtulia

"Nichagueni nikahakikishe Vijana wanakopeshwa bodaboda, wanasajiliwa na wanapewa namba ya utambulisho" - Mtulia

"Nichagueni nikasimamie Vijana na akina Mama wanapewa haki yao ya mikopo ya asilimia 10 ya mapato toka Manispaa" - Mtulia

"Nichagueni nishirikiane na Serikali nihakikishe wana Kinondoni wanatoka kwenye mfumo kwa kupewa leseni ya makazi ya miaka 3 na kuanza kupewa hati ya miaka 99. Serikali ipo tayari kuwapa hati zenu." - Mtulia

Maoni