ZIJUE FAIDA ZA MIWA NA JUICE YAKE KIAFYA.

Inafurahisha kuona kuwa wapo wafanyabiashara wengi sehemu nyingi nchini wanaouza juisi ya miwa ama miwa yenyewe.

Kimsingi juisi hii ni sukari halisia ambayo haijachakatwa. Sukari halisia ni nzuri kwa mwili kwani ina virutubisho na madini kwa wingi. Miwa ina faida nyingi kiafya. Juisi ya miwa inafahamika na wataalamu wa afya kwa kuwa na uwezo wa kuupa mwili nguvu kwa sababu ya ‘glucose’ iliyopo.

Kijiko kimoja cha juisi ya miwa, kina calories 11. Madini halisi na vitamin zinazopatikana katika sukari ni kama phosphorus, calcium, madini ya chuma na potassium.

Si hivyo tu, miwa ni jamii ya mmea lenye alkali hivyo lina uwezo wa kupambana na saratani hasa ile ya kibofu cha mkojo na saratani ya maziwa.

Miwa ina upekee wake kwani ina uwezo wa kuongeza maji mwilini, inaupooza mwili na kuupa nguvu.Virutubisho vilivyopo katika miwa vina manufaa makubwa katika

kusaidia utendaji kazi wa ogani muhimu kama figo, moyo, ubongo na viungo vya uzazi.

Pia, wagonjwa wa kisukari wasihofie sukari iliyopo kwenye miwa kwani haina madhara yoyote kwao.kwani aina ya sukari iliyomo kwenye mua (sucrose) ni non reducing au complex sugar. Uzuri wa juisi ya miwa ni kuwa sukariyake ni halisia.

Chanzo: Doctor Joh

Maoni

Chapisha Maoni