ABIRIA WANUSURIKA KIFO KUFUATIA KUPINDUKA KWA BASI LA KIMOTCO NDANI YA MTO

Basi la Kampuni ya Kimotco (pichani) lililokuwa likitoka Musoma,kwenda Arusha kupitia Mugumu,limepinduka katika mto unaodaiwa kuwa na viboko ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo William Mwakilema amethibitisha kupata taarifa ya tukio hilo leo Machi 16,na kusema kuwa katika ajali hiyo hakuna majeruhi wala vifo,na kuwa abiria wote wako juu ya basi.

Jitihada za kuwaokoa mmoja mmoja zinaendelea.Baada ya basi hilo kusombwa na maji abiria wote walitokea juu ya madilisha ya basi na kukaa juu yake,kwani halikuzama lote,jitihada za kuwaokoa zinaendelea  mpaka sasa,ambapo zaidi ya abiria wanne  wametolewa.

TAARIFA ZAIDI TUNASUBIRI KUTOKA MAMLAKA HUSIKA 

 Baadhi ya abiria wakiwa juu ya basi hilo mara baada kupinduka,wakiokolewa mmoja mmoja na Lori kama ionekavyo pichani

Basi likiwa limepundika kwenye mto ndani ya hifadhi ya serengeti.

Maoni