AJALI YAKATISHA MAISHA YA MWALIMU


Aliyekuwa Mwalimu wa shule ya sekondari ya St.Mary’s iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Hipoliti Julius Milambo amefariki dunia papo hapo baada ya kogongwa na gari aina ya Hiace.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo,marehemu aligongwa jana majira ya jioni na gari linalotajwa kuwa lilikuwa likitoka kata ya Kakese ambapo aligongwa na gari hilo wakati akivuka barabara.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Dkt.Theopister Elisha akizungumza na Mpanda Radio Ofisini kwake amesema hajapata ripoti ya kifo cha mwalimu huyo.

Hata hivyo kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda alipotafutwa kuelezea tukio hilo amedai kuwa yupo msibani.

Waendeshaji wa vyombo vya moto wameshauri kuwekwe matuta katika barabara Mpanda - Kigoma ili kupunguza ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikitokea.

Chanzo:Isack Gerald

Maoni