ATAKA KUJIRUSHA KUTOKA JUU YA MNARA BAADA YA KUAMBIWA LOWASA KAFUNGWA

Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Maneno amenusulika kifo baada ya kupanda kwenye mnara wa simu za mkononi hadi kileleni na kukaa kwa muda wa saa 9 bila msaada wowote wa uokozi kutoka mamlaka husika.
Tukio hilo limetokea jana.

Wakizungumza baadhi waliozungumza naye akiwa juu wamedai kuwa amechukua uamuzi huo kwa madai kuwa amesikia kwenye vyomba vya habari kuwa,
amehukumiwa kifungo jela, taarifa ambazo si za kweli, bali ni taarifa ya Mbunge wa Mbeya Mjini, ambaye amehukumiwa kifungo za miezi 5 jela. 

Edward Lowassa
Joseph Mbilinyi
Mwenyekiti Wa Kijiji cha Mtakuja Kata ya Buseresere Wilaya ya Chato mkoani Geita, Varely Kakonko amedai kuwa kijana huyo anaekadiriwa kuwa na miaka 24-26 ana matatizo ya akili na jaribio hilo siyo la kwanza kutokea kwani awali alishawahi kufanya jaribio kama hilo.

Kijana huyo amekaa katika kilele cha mnara huo zaidi ya saa 9 hadi alipoamua kushuka kwa hiari yake majira ya saa 12 jioni ambapo tayari jeshi la Polisi kwa kushirikiana Jeshi la Zimamoto na Uokozi walimchukua mtu huyo hadi Kituo cha Buseresere kwa uchunguzi zaidi.

Maoni