AZAM FC KUANZA MAZOEZI WAKIMSUBIRI MTIBWA SUGAR.

Na Agness Francis Globu ya jamii.

KLABU Bingwa Afrika Mashariki na kati Azam FC kesho wanatarajia kuanza rasmi mazoezi ili 

kujiandaa zaidi na michuano ya kuwania Kombe la Shirikisho (ASFC) 

 ambapo watavaana na Mtibwa Sugar katika mchezo huo wa mtoano.

Mchezo huo utakuwa ni wa vuta nikuvute ikiwa kila timu ikihitaji kupata matokeo mazuri ili kusonga mbele zaidi.  Mchezo huo utarindima katika 

dimba la Uwanja Wa Azam Complex Chamazi Machi 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam huku Azam akimkaribisha Mtibwa Sugar .

Ofisa Habari  Azam FC Jaffary Iddy amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa baada ya kumaliza mchezo wao wa Ligi dhidi ya Mbao FC ambapo walipata ushindi wa mabao 2-1, kikosi kilikuwa kwenye mapumziko na kesho kinaaanza mazoezi rasmi ili kukabiliana  na mchezo wao ujao dhidi ya Mtibwa sugar.

Ambapo katika mtanange huo ataeibuka kidedea ndiyo ataingia Nusu Fainali ambapo Jaffary amesema wanatarajia mchezo kuwa mgumu  kwa pande zote mbili kuwa na morali ya kupata ushindi wa aina yoyote ili kutinga fainali na  kusonga mbele.

 "Mchezo utakuwa mgumu kwa pande zote mbili tunafahamu timu ya Mtibwa na ikiwa kila kikosi kinahitaji ushindi ili kuendelea na mashindano ukizingatia katika mchezo huo lazima mmoja atoke na mwengine asonge mpaka kufikia kilele na kupata mshindi ambaye atakuwa ni muakilishi wa Nchi  kombe la shirikisho Barani Afrika,"amesema Jaffary. 

Ameongezea  vijana wapo vizuri  isipokuwa katika mchezo huo watawakosa wachezaji wao Danile Amor(Ghana)na  Yakubuku Mohamedi ambao ni majeruhi pamoja na Yahya Zayd aliyeitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars.

Maoni