BAMIA TUPO TAYALI KUWAANGAMIZA KISEWE QUEENS

Na shabani rapwi

-Mach 16, 2018.

Kikosi cha Bamia Queens kiko tayali kukivaa kikosi cha Kisewe Queens hapo Jumamosi Mach 17, 2018 kwenye uwanja wa Kisewe, Saa 10 Jioni.

Kuelekea kwenye mchezo huo RapwiNews imemtafuta Katibu Hamasa na Chipukzi wa tawi ilo la Bamia, Maryam Muki na kufunguka yafuatayo 

"wadau tunaomba dua zenu kwenye mchezo wetu dhidi ya Kisewe ili tushinde"

Akaendelea kwa kuwataka wachezaji wa pande zote mbili kucheza vizuri na kwa amani kwani michezo ni amani,upendo na furaha.

Kwa upande wa kocha wa timu hiyo Aisha Baby amewataka wachezaji wake kupambana ili waweza kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo.

"nawaomba tu wachezaji wangu wapambane ili tupate ushindi jambo ni mchezo mgumu sana kwetu kwani Kisewe tunaifahamu na walishatufunga kwenye mchezo wa awali rakini hii isiwakatishe tamaa wachezaji wangu wapambane tu" alisema Aisha.

Maoni