BITEKO: TUFANYE SIASA ZA MAENDELEO KWA WANANCHI

Na Mathias Canal, Geita

Wanasiasa hasa wasomi na wale wenye ushawishi mkubwa nchini wametakiwa kuacha kulalamika na kutoa kauli ambazo hazitawasaidia wananchi katika kuwatatulia matatizo na kero zao bali waungane na serikali katika juhudi zinazoonekana za kuleta maendeleo. 

Rai hiyo imetolea na Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi uliofanyika katika Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo akiwa katika ziara ya kijimbo ya siku nne.

Mhe Biteko amesema baadhi ya wanasiasa maarufu wamekuwa wakitumia muda mwingi kueleza matatizo na kero za wananchi bila ya kuonyesha suluhisho au kusaidia kutatua kero hizo jambo ambalo halimsaidii mwananchi kwa namna yoyote.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo Mkoani Geita wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwa katika ziara ya Kijimbo kusikiliza kero za wapiga kura wake, Jana 3 Machi 2018.

Pamoja na mvua kunyesha lakini baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo Mkoani Geita wakifatilia kwa karibu na umakini mkubwa mkutano ulioitishwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati akiwa katika ziara ya Kijimbo kusikiliza kero za wapiga kura wake, Jana 3 Machi 2018.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwaeleza Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo Mkoani Geita waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara juu ya namna bora ya kuwa na mafanikio kama Taifa kwa kufanya kazi kwa bidii, Jana 3 Machi 2018.

Maoni