CCM YALETA NEEMA KWA BAJAJI NA BODABODA MBEYA JIJI

Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Mbeya ameushukuru uongozi wa Ccm Mkoa   na wilaya kwa ujumla kwa kumaliza matatizo ya vijana wa Bodaboda na bajaji katika jiji la mbeya,ambapo katika kikao hicho cha ndani kiliuzuliwa na uongozi wa ccm mkoa na wilaya, mkuu wa wilaya mbeya jiji,kaimu  mkurugenzi wa jiji mbeya,msaidizi wa OCD mbeya, wakuu wa idara Sumatra, wakuu wa idara halmashauri ya jiji, wakuu wa usalama barabarani mkoa na wilaya,viongozi wa bajaji na Bodaboda.

Katika kikao hicho ni muendelezo aliouacha katibu wa Nec siasa,itikadi na uenezi ndg polepole kwa viongozi wa mkoa na wilaya. 

Baada ya majadiliano mazuri na serikali yetu sikivu utekelezaji Umeanza mara Moja 

Barabara ya Isanga -kabwe imeanza kutengenezwa na mkandarasi yupo site Sasa pamoja na baadhi ya Barabara kadhaa ndani ya jiji letu.

Ukamataji holela wa bajaji na Bodaboda sasa uzingatiwe sheria. 
Bajaji na Bodaboda kuomba vituo karibu na stand.

Mikopo kwa vijana Hasa 4% zinazotoka katika halmashauri zetu.

Katika Kikao hicho pia mdau wa maendeleo mkoa wa mbeya Ndg NDELLE MWASELELA aliwachangia mil 6,000,000 ili vijana wa bajaji na Bodaboda waweze Sasa kujiendesha vzr ndani ya vyama vyao.

Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa ameushukuru Sana uongozi wa chama mkoa na wilaya kwa kuwa wasikivu na Wapenda maendeleo,
Pia tunamshukuru mkuu wa wilaya kwa kusimamia vyema utekelezaji huo ulioenda vzr kabisa kiutendaji. 



Imetolewa na idara ya Habari.
UVCCM (M) 
Soko matola
Mbeya.

Maoni