CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAIELEKEZA SERIKALI KUFUTA MARA MOJA TOZO KUBWA ZILIZOANZISHWA NA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI KWA WAFANYABIASHARA WA KIGOMA.

18 March 2018

Katika Mkutano wa Halmashauri Kuu maalumu ya Wilaya ya Kigoma Mjini, CCM kupitia kwa Katibu wa Nec, Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole kimeielekeza Serikali kufuta mara moja tozo kubwa zilizoanzishwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa wafanyabiashara Kigoma.

Akizungumza na wajumbe wa halmashauri Kuu  Maalumu ya CCM ya Wilaya ya Kigoma Mjini, Viongozi wa CCM, wanachama wa CCM, Viongozi wa Serikali na watumishi wa Halmashauri kutoka Wilaya za Uvinza, Buhigwe, Kigoma Vijijini na Kigoma Ujiji pamoja na wafanyabiashara wa Kigoma ujiji Ndg. Polepole amesema tozo kubwa zisizo zingatia haki kwa wanafanyabiashara ni kinyume kabisa na Imani ya CCM, Sera za CCM na Ilani ya uchaguzi ya CCM Mwaka 2015 - 2020 inayotekelezwa sasa.

"Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Rais na Mwenyekiti wa CCM anawapenda sana wafanyabiashara na anapenda wafanye biashara zao vizuri na walipe kodi zinazo zingatia haki kulingana na kipato chao, haiwezekani kwa kukosa kwenu ubunifu wa kuongeza vyanzo vya mapato mnawakomalia wafanyabiashara hawa walipe tozo kutoka Tshs. 15000 hadi Tshs. 50000 siyo haki". amesisitiza Ndg. Polepole


Uamuzi huu umefikiwa baada ya mgogoro uliyodumu kwa takribani mwezi mmoja baina ya wafanyabiashara na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma ujiji uliyopelekea kufungwa kwa maduka ya biashara jambo ambalo limeshabisha usumbufu mkubwa kwa wananchi kwa kukosa huduma na mahitaji ya msingi.
  
Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA  CHA MAPINDUZI (CCM)

Maoni