DC GODWIN NGONDWE AWATAKA VIJANA KUWA CHACHU YA MAENDELEO.

DC wa wilaya ya Handeni na Kaimu DC  wilaya ya Korogwe Mh Godwin Ngondwe Jana Machi 21,2018, alitembelea tawi la Vijana Uvccm Chuo cha Ualimu Korogwe na alizungumza na Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  waliopo katika Chuo Cha  Ualimu Korogwe, Msafara wa DC Gondwe  aliambatana na Mkurugenzi wa wilaya ya Korogwe mjini Ndg. Jumanne Shauri,na DSO wilaya ya Korogwe Ndg  Maswi. 

Akizungumza na Vijana wa Chuoni hapo Mh DC Gondwe  aliwataka vijana hao waisemee Serikali kwa wananchi katika jamii zao,juu ya mambo mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano iliyochini ya Rais mtiifu DK JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI, pia DC  Gondwe aliwataka vijana hao wakawe chachu ya maendeleo katika jamii zao mara wanapohitimu masomo yao,kwani wakiwa kama vijana ni tegemeo katika jamii zao na Taifa kwa ujumla. 

alisema "vijana ni tegemeo la leo na kesho,vijana uwe imara na msiwe goi goi katika jamii yenu".  
Aliwaasa vijana kutojihusisha na makudi yanayotaka kuvuruga amani ya nchi yetu,na aliwataka vijana hao wawe walinzi wa amani katika taifa letu na aliwataka vijana kutokua wavivu,na wafanye kazi kwa kujituma pasipo kuchagua kazi.

  "vijana pendani kujiajili wenyewe pasipo kutegemea zaidi kujiajiliwa". Alisema DC Gondwe 

Nae Mwenyekiti wa UVCCM tawi la Chuo Cha Ualimu Korogwe Ndg. George Madaraka alimshukuru DC Gondwe Gondwe kwa kuacha shuguli zake na kuja kuwatembelea vijana. 

"Kwa  ujumla Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  Chuo Cha Ualimu Korogwe wamefarijika sana na ujio wako DC  Gondwe na tunayalihahidi kuyapokea yote ulio yazungumza Mh DC  na kwenda kuyafanyia kazi kwenye jamii yetu" Alisema Ndg Madaraka. 

Pia Mwenyekiti huyo alito shukrani kwa  Mh  Rais Dk John Joseph Pombe Magufuli kwa niaba ya Vijana wa Chama  Cha  Mapinduzi  Chuo Cha Ualimu  Korogwe kwa kumteua Mh Godwin  Gondwe kua Mkuu wa wilaya ya Handeni na kua Kaimu DC wilaya ya Korogwe kwani anaendana na kasi na Serikali ya awamu ya tano.

Maoni