DIWANI AFUNGUA MASHINDANO YA UVCCM MIBURANI CUP 2018.

Diwani wa Kata ya Miburani Ndg. Juma R Mkenga alipokuwa akifungua Mashindano ya Uvccm Miburani Cup 2018,Mar 03,2018  katika uwanja wa Buliaga Jijini Dar es Salaam.

Mkenga alisema anatumaini kuwa Kata zingine zitaiga mazuri yanayofanywa na UVCCM kata ya Miburani. 

"Niwapongeze sana vijana wangu kwa kazi nzuri mnavyo ifanya ya kuamasisha vijana wenzenu na kukifanya chama cha mapinduzi kinakuwa bora na imara kwa vijana wa Kata hii ya Miburani" alisema Juma Mkenga

Kwa upande wake Katibu UVCCM kata ya Miburani Ndg. Swaumu Chollah alimshukuru Juma Mkenga kwa kuitikia wito wa kuja kufungua Mashindano hayo na alimtaka azidi kuwa mlezi wa Kata ya Miburuani katika maswala yote yanayohusu maendeleo ya Chama Cha Mapinduzi Jumuhiya ya Vijana.

"Nimefurahi sana Diwani kuitikia wito huu wa kuja kufungua Mashindano haya   nakushukuru sana na ushirikiano huu Mh Diwani uzidi kuwa endelevu kwetu vijana" alisema Swaumu Chollah

Mh Diwani akiwasalimia wachezaji wa timu ya Miburani Queens. 

Mh Diwani akiwasalimia wachezaji wa timu ya Wailes Queens. 

Mh Diwani akiwasalimia wachezaji wa timu ya Uwanjan wa Taifa fc. 

Mh Diwani akiwasalimia wachezaji wa timu ya Miburani Fc. 

Mjumbe wa k/siasa wilaya ya temeke Ndg.  Happy Nasilika Nyema Nyema akiwasalimia wachezaji wa timu ya Uwanja wa Taifa Fc. 

Baada ya Mh Diwani kufungua Mashindano hayo,kulipigwa mechi mbili kali moja ikiwa ya footbali na mchezo mwingine ukiwa wa rede

Mchezo wa mwanzo ulikuwa wa Rede ambao ulizikutanisha timu ya Miburani Queens na Wailes Queen ambao ulichezwa kwa dakika 40 kila kipindi iki  dakika 20.

Mpaka dakika 40 za mchezo huo una kamilika Miburani Queens 1-1 Wailes Queens.

Na Mchezo uliofuata ulikuwa wa footbali ambao ulikuwa mkali na wa ushindani mkubwa ulio zikutanisha timu ya Miburani Fc dhidi ya Uwanja wa Taifa Fc mpaka dakika 90 za mwamuzi zinakamilika Miburani Fc 4-1 Uwanja wa Taifa. 

Katika mchezo huo Abirahi Rashidi aliyekuwa mwiba kwa Uwanja wa Taifa Fc alipiga Hat-Trick na kukabiziwa zawadi ya mpira na Mjumbe wa Siasa wa Wilaya ya Temeke Ndg Mussa Mtulia alimwongezea shiling Elfu Kumi 

(10,000/=)

Abirahi akikabidhiwa Mpira na Mjumbe wa Siasa wa Wilaya ya Temeke Ndg Mussa Mtulia.

Baada ya kumkabidhi mpira huo Ndg Mussa Mtulia alimpongeza Abirah kwa kucheza vizuri na kwa nidhamu ya hali ya juu na kuwataka vijana wengine kuiga mfano wake.

Imetolewa na 

Afisa habari Ally kiaka 

kata ya miburani. 

Maoni