EFM REDIO YAWAWEZESHA KINAMAMA.

 Efm redio katika kuadhimisha siku ya wanawake ambayo huadhimishwa duniani kote tarehe 8 machi kila mwaka, imetimiza jukumu iliyojipatia kuwasaidia wanawake wanaolea watoto wao wenyewe “single mothers” bila msaada wa wazazi wenza kwa kuwapatia mahitaji mbalimbali kama mtaji katika kuendeleza biashara zao ndogondogo.

Kampeni hii iliobeba kauli mbiu ya “hatupoi” ilianza mwezi wa pili katika siku ya wapendanao, ambapo Jumla ya wanawake 19 wamefanikiwa kuwezeshwa.

Vilevile Efm redio imetoa hamasa kwa jamii hususani wanawake kuto chagua kazi ili kuleta usawa wa kazi katika jamii kwa kuwatambua na kuwakabidhi wanawake baadhi hati maalum ya utambuzi kama “wanawake wa shoka”. kwa uthubutu wao wa kufanya kazi ambazo wanawake wengi wamekua wakiziogopa kutokana na ugumu wake na imani iliyoko ndani ya jamii kuwa kazi hizo hufanywa na wanaume pekee.

 Kulia ni Meneja matukio wa efm redio Jesca Mwanyika akikabidhi vifaa vya biashara ya juisi ikiwa ni friji na Brenda kwa bi. Siwatu Mathew

  Mmoja wa single mother akikabidhiwa pesa taslimu kiasi cha shilingi 250,000/= na Afisa habari wa Efm radio Tuyu Mwaleni

 Fundi selemala Bi. Evodia Eliya akipokea cheti cha utambuzi kama “mwanamke wa shoka” kwa uthubutu wake katika kazi

 Mjasiliamali wa kuuza mbogamboga akikabidhiwa Kiasi cha shilingi  250,000/= katika kukuza mtaji wake wa biashara.

 Mjasiliamali wa biashara ya chakula cha kuku (kulia) akikabidhiwa na Afisa habari Efm redio Eunice Yona Mzani na mifuko miwili ya chakula cha kuku katika kuelendeleza mtaji wake.

Maoni