GRACE MUGABE MATATANI, ACHUNGUZWA SASA KWA "UMALKIA WA MENO YA TEMBO"

Grace Mugabe, mke wa Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe anachunguzwa kwa shutuma kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo.

Uchunguzi huo umeanzishwa baada ya uchunguzi mwingine mkubwa uliofanywa kwa kipindi cha miezi mitatu na mpiga picha wa masuala ya wanyamapori MuAustralia, Adrian Steirn.

Katika mahojiano maalum na Al Jazeera, Steirn amesema aliling'amua genge la majangili na wauzaji alipoanza kutafiti juu ya biashara haramu ya uuzaji meno ya tembo kuanzia Desemba mwaka jana.

"Meno ya tembo yalikuwa yakitoka aidha kwenye ghala la uhifadhi la taifa, kwa kuyaiba ama kwa genge la majangili kuwauwa moja kwa moja tembo kisha kuyauza kwa kundi la Grace Mugabe," amebainisha Steirn.

Anaongeza kwamba, Grace akishauziwa yeye aliyafungasha na kuyapeleka uwanja wa ndege. "Kitu chochote katika uwanja wa ndege ikiwa ni mali ya mke wa rais, ilikuwa haikaguliwi kwa namna yoyote."

Steirn amekusanya ushahidi wa picha mnato na video na aliounesha Al Jazeera. Anasema ushahidi wote huo unaonesha namna mke wa Mugabe alivyokuwa akijihusisha kwenye biashara hiyo haramu.

Biashara ya meno ya tembo inafanywa kwa udhibiti nchini Zimbabwe lakini hayaruhusiwi kuuzwa nchi za nje.
Katika majibu yake kuhusu sakata hilo, Christopher Mutsavangwa, Mshauri Maalum wa Rais Emmerson Mnangagwa amesema serikali ya Zimbabwe itatafuta majawabu kutoka pande zote ikiwemo kwa Grace Mugabe kuhusu namna wanavyoelewa usafirishaji haramu wa meno hayo katika mataifa ya nje, jambo ambalo ni mwiko nchini humo.

Watu wawili wamekamatwa kwa kosa la utoroshaji wa meno ya tembo.

Watu wa karibu na Grace bado hawajajibu shutuma hizo akiwemo mwanasheria wake.
Katika utawala wa mumewe, Grace alikuwa katikati ya duara ya mazungumzo na minong'ono mingi kutokana na mtindo wake wa maisha na manunuzi ya kifahari hadi kuitwa "Gucci Grace"
Mwezi Desemba mwaka jana baada ya Mnangagwa kuchukua hatamu za uongozi meno ya tembo yenye uzani wa kilo 200 yaliyokuwa yakisafirishwa kwenda nchini Malaysia yalikamatwa na kuzuiliwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe. 

Katika ushahidi mpya wa Steirn, anasema meno hayo pia yana mkono wa Grace Mugab

Maoni