JIKO LA GESI LAZUA KIZAA ZAA MJINI BABATI

Mtu mmoja anaesemekana kuwa ni daktari wa hospitali ya mkoa wa Manyara amenusurika kifo baada ya jiko la gesi alilokuwa akilitumia chumbani kwake kulipuka hali iliyopelekea moto mkubwa kuwaka katika chumba hicho.

Tukio hilo limetokea usiku wa March 14.2018 katika mtaa wa Nyunguu mjini Babati.

Licha ya watu kujitokeza kumuokoa,aliendelea kujifungia chumbani kwake na kuwapiga walikuwa wakimpa msaada lakini wakafanikiwa kuuvunja Mlango na kumtoa mtu huyo ambaye alionekana amelewa.

Hata hivyo jeshi la zimamoto na uokoaji walifika kwa wakati katika eneo la tukio na kuuzima moto huo na kumpeleka katika kituo cha polisi.

Tanesco walizima Umeme kwa dakika 20,toka saa 2;30 hadi saa 2:40 usiku kukwepa madhara kutokea zaidi.

Chanzo:  W.  Habari. 

Maoni