JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA MOROGORO YAZITAKA WILAYA ZOTE KUJIIMARISHA KIUCHUMI KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 41 YA CCM WILAYANI MVOMERO

Mhe Mansuet alizitaka wilaya zote za mkoa huo zijiimarishe kiuchumi kwa kuanzisha miradi mbalimbali ili ziweze kujitegemea kiuchumi. Katika ziara hiyo ambayo kamati ya utekelezaji mkoa ilifika pamoja na ndg Adolf Milunga ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya uchumi ya jumuiya hiyo mkoa wa Morogoro.Mgeni rasmi alipokelewa katika ofisi za chama wilaya ya mvomero na kutembea mwendo wa miguu hadi kwenye kituo cha watoto walemavu na kutoa misaada ya kijamii wakiongozwa na katibu wa wazazi wilaya ya Mvomero ndg Ally Kibwana
Baadae mgeni rasmi alizungumza na viongozi wa chama na jumuiya ya wazazi tarafa ya mvomero
Kutoka ofisi ya jumuiya ya wazazi (CCM) mkoa wa MOROGORO
Maoni
Chapisha Maoni