KATIBU HAMASA NA CHIPUKIZI KATA YA CHAMAZI, AANDIKA HAYA BAADA YA DIAMONDI KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKYEMBE,BASATA KWA MASAA MATATU

Katibu Hamasa na Chipukizi kata ya Chamazi Ndg. Najim Nyanza, ameandika kupitia ukurasa wake wa Facebook leo hii, baada ya hapo jana  Diamond Platnumz, kukutana na Dr.Harrison Mwakyembe,Mh.Juliana Shonza  kumaliza tofauti zao.

Kwenye ukurasa wake wa Facebook, Nyanza kaandika kama ifuatavyo. 

"Juzi tu, mlimcheka Diamond na kumuona kazingua na ndio mwisho wake umefika.

Na mkasema kua aliimba "NIKAE KIMYA" sasa akome.

Eti leo mnasema kwa nini aitwe Peke yake?? Mbona mlimsimanga Peke yake??

MY TAKE
Unapomzungumzia Diamond Platnumz basi unazungumzia Icon kubwa ya Muziki si Tanzania tu bali Africa na Dunia kwa ujumla so inapotokea kuna misunderstanding kati ya serikali na mwanamuziki mkubwa kama huyu si dhambi kuketi nae chini na kufanya nae mazungumzo hii ni kwa maslahi mapana kwa nchi yetu changa. Pia nichukue fursa hii kupongeza pande zote mbili kwa maana diamond platnumz na wizara husika kwa busara kubwa walioitumia kuhakikisha hili suala linaisha tena kwa wakati na hii ndio Tanzania ambayo kila mtanzania anataka iwe.#Cheerz" - Najim Nyanza

Maoni