KATIBU UVCCM WILAYA YA UBUNGO, Bi. LEAH D. MBEKE AFUNGUA BONANZA LA PASAKA UVCCM KATA YA SARANGA.

Na Mwandishi wetu, SARANGA.

Siku ya leo vijana wa Kata ya SARANGA wameanza bonanza la pasaka linaloisha siku ya kesho. Bonanza hilo limeandaliwa na viongozi UVCCM kata ya saranga wakiongozwa na mwenyekiti wa UVCCM kata ya Saranga,ndugu KELVIN KITASO.

  Vijana hao wamefunguliwa bonanza hilo na katibu wa uvccm wilaya Bi. LEAH D. MBEKE ambaye ndiye aliyealikwa kuwa mgeni rasmi wa bonanza hilo. Pia aliambatana na wajumbe wa baraza la uvccm Ubungo ambao ni Mwenyekiti uvccm Kata ya Kimara,ndugu. CLIEFF MTAPAI pamoja na katibu wa uhamasishaji kutoka kata ya Msigani ndugu,WINIFRIDA ANTHONY.

Bonanza hilo lililokuwa limejaa hamasa na bashasha za kila namna ambazo zilimfanya katibu huyo kutoa neno TIMU 11 zenye jumla ya wachezaji 121 zilizokuwa zinachuana Kwenye bonanza hilo.
"Hongereni sana kwa bonanza zuri,kwakweli nimefurahi kukutana nanyi na napenda nikutane nanyi kwa mazungumzo zaidi siku ya tarehe 14/04/2018 ofisini kwangu,nitaanda kitu kidogo kwa ajili yenu kuonesha kuwa katika kila jambo zuri ambalo vijana wanafanya katibu wenu sitasita kuwaunga mkono na tutapambana pamoja kwenye shida na raha,tutacheka wote na tutalia wote!." alisema katibu huyo.

Maoni