KATIBU WA CCM WILAYA YA NJOMBE AWAONGOZA UVCCM NA JUMUIYA YA WAZAZI NGOGO, KUWAJENGEA UWEZO WA MIPANGO NA UCHUMI KATA ZA LUGENGE,UTALINGOLO NA LUPONDE 


Imetolewa na Titho stambuli na Erasto kizumbe kutoka ofisi ya siasa na uenezi mkoa wa Njombe.

HAPA KAZI TU, kwa wengine ni Msemo tu lakini, CCM Wilaya ya Njombe na Jumuiya zake imeonekana kuupokea kwa vitendo. 

ungeweza kuwaza hali ya hewa ni kikwazo kuzunguka wilaya ya Njombe ! Mbinu nzuri unaweza ipata kwa katibu wa wilaya Hiyo na kamanda wake Daniel Muhaza na Ngogo-wazazi. 

Ilikuwa mida ya saa mbili ndipo rubani wetu Mahenge alipoanza kupasua anga kuitafuta lugenge licha ya barabara kuharibiwa na magari makubwa umahiri mkubwa wa Rubani wetu Mahenge hakushindwa kuwafikisha wataalamu hao lugenge. 

Ndege ilipotua lugenge Ndugu zetu walitupamba kwa nyimbo na mapambio walipoona wageni wao wamevalia masharti ya kijani waliamimi leo pia ni siasa ya kuimba na hakika waliimba....... iyena......... iyena iyena.........,lakini mkoba uliobebwa na Daniel Muhaza -katibu uvccm wilaya ya Njombe haukugundulika kwa haraka umebeba nini. 

Watalamu hao wa ccm walikaribishwa ofisini kila mmoja alionekana na tabasamu baada ya kuonana na viongozi wa wilaya, cha kushangaza begi letu lilikuwa na chaki na karatasi zenye jedwari, hapa hata Mwandishi nilianza kuhisi kukumbushwa hesabu za shuleni lakini swali langu likawa wanasiasa mahiri Kama hawa watazirudi hesabu Kweli?. 


Lengo la hesabu hizo ilikuwa ni kuwajengea uwezo viongozi wa kata hizo ilikuweza kuboresha mipango na uchumi ya ccm ndani ya Kata hiyo. 
Viongozi hao wameonyesha umahiri mkubwa katika kutoa somo la ubunifu,mipango na usimamizi wa miradi, ukiachana na siasa hawa viongozi mahiri Sana wa hesabu, Katibu wa ccm wilaya ya Njombe Antony katani ameonesha umahiri wa kukokotoa hesabu, huku katibu wa uvccm wilaya ya Njombe -Daniel Muhaza akinogesha Darasa hilo kwa kuwa na uwezo mkubwa wa ubunifu na usimamizi wa miradi,Huku somo hilo likaonekana kunoga pale mzee wa mipango Ngogo -wazazi, alipoonyesha ni jinsi gani unaweza kuwa na mipango ya kutafta fedha. Hakika ccm wilaya ya Njombe tunaviongozi wenye vipawa tunahitaji kujifunza mengi kwao zaidi.

Watalaamu hao wamenyesha nia yao ni kuhakikisha kata zote zinakuwa na budget elekezi ya kiutendaji katika kata hizo na ili kufanikisha zoezi hilo ni lazima watoe mafunzo kwa viongozi waandamizi na wasimamizi wa kata hizo. Na uwezo wa kubuni miradi itakayo weza kuwapatia fedha kwa kuendesha mpango huo, Kwani wanaamini ccm ili iwe na nguvu ni lazima hali ya uchumi iwe nzuri ili kuweza kufanikisha mipango mbalimbali ndani ya Kata hizo na kufanya chama kiwe na nguvu, pia kufanya shughuli zakijamii zitakazo kuwa zinajitokeza katika maisha yetu ya kila siku. 


Pia wameweza kuwapa somo ili kuweza kufanikisha mpango wa kupata fedha ni lazima wazitumie fursa zinazo wazunguka ili kuweza kupata fedha mfano kilimo cha parachichi, mahindi, miti, na kutumia vipawa walivyonavyo ambavyo vitatumika kama fursa ya kuongeza kipato kama vile kushona vikapu, michezo na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali. 

Amewakumbusha pia namna ya utunzaji wa nyaraka Za taarifa za matumizi ya fedha akikazia kwa kusema "mali bila daftari huisha bila habari".

Nao viongozi wa kata hiyo wameonyeshwa kufurahishwa namna ambavyo viongozi hao wameweza kufika kutoa maelekezo hayo, wameahidi kuyafanyia kazi na kwa ustadi mkubwa kwani wanaamini utendaji mkubwa wa chama unahitaji kuwa na fedha hivyo ni lazima wawe na mipango na ubunifu wa upatikanaji wa fedha. 


Maoni