KATIBU WA CHADEMA ARUSHA AJIUNGA NA CCM.

Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema ) Wilaya ya Arusha Mjini Ndg.Gabriel Lucas Kivuyo Ametangaza Kujivua nafasi zake zote na kujiunga na Ccm.

Akitangaza kujivua Uanachama huo na nyadhifa zote alizo kuwa nazo ndani ya Chadema amesema ameamua kwa moyo wake mkunjufu ppkumuunga mkono Mh Rais magufuli katika kulijenga Taifa na kusimamia Rarisilimali za nchi hivyo hana sababu ya kubaki CHADEMA wakati yote waliyokuwa wanayaamini sasa yanatelekezwa na CCM hivyo ameamua kujiunga na Ccm
Katibu huyo amepokelewa na Katibu wa Wilaya ya Arusha Mjini Ndg. Mussa Matoroka na Katibu mwenezi wa Wilaya ya Arusha Mjini Ndg.Abrahamu Mollel pamoja na Katibu Hamasa wa Vijana Mkoa wa Arusha Ndg. Omary Lumato

Maoni