KATIBU WA HAMASA NA CHIPUKIZI UVCCM MKOA WA NJOMBE  , AWAFAGILIA UWT MKOA WA NJOMBE KWA MAPOKEZI MAKUBWA YA VIONGOZI WA KITAIFA WA UWT .

Katibu huyo aliyeonekana kutikisa anga za makambako Wiki mbili zilizopita , ambapo alifika Kutetea maslahi ya vijana wake ambao ni madereva Bodaboda, Bajaji na watumiaji wa huduma hiyo.

Ameibuka tena na kuwafagilia UWT mkoa wa Njombe kwa kazi nzuri inayoashiria mshikamano ndani ya Umoja huo, Ndg. Johnson Elly Mgimba ambaye alishiriki kuupokea ugeni huo mzito wa UWT, ambao ulikuwa na  viongozi waandamizi watatu Mwenyekiti wa UWT
Taifa Bi Gaudensia Kabaka, Katibu mkuu na Naibu katibu mkuu,Kila kiongozi alitembelea maeneo tofauti, Huku Naibu katibu mkuu -Eva kihwele akiongozana na Katibu wa hamasa na chipukizi mkoa wa Njombe Ndugu Johson Elly Mgimba kuelekea kufanya ziara wilaya ya ludewa ,ambako ndiko nyumbani kwa katibu hamasa huyo, haikumpa shida kuzijua njia za wilaya hiyo na kuungoza msafara vyema.

Alionekana na Furaha kwa mapokezi ambayo yamefanyika akiwa njombe, huku akiwaza je na kwao Ludewa mapokezi yatakuwa ya Nguvu. 

 Mshangao Mkubwa alivyopokelewa yeye na mgeni huyo ni mapokezi ya aina yake na kumfanya awe na furaha zaidi na kuwapa tano UWT.


Mapokezi tuu haikutosha bali namna ambavyo UWT wamemuonyesha Naibu katibu mkuu umahiri mkubwa wa kushiriki shughuli za kijamii,kuhamasisha  akina mama kuwa na miradi ya kiuchum, kuwajengea uwezo wa Kukopa fedha halmashauri, na kuwapa semina ya ujasiriamali wanawake wilayani ludewa .

Licha ya kujionea umahiri wa UWT wilayani ludewa aliweza kufuatilia matukio kwa ukaribu sana kutoka wilaya nyingine yaliyokuwa yakirushwa moja kwa moja kwa udhamini wa shikamooparachichi, alipata kuhabarika vyema na kukiri kuwa UWT ni jeshi kubwa. 


Akiongea kwa Njia ya simu na mwandishi kwamba anawaasa jumuiya nyingine kujipanga na Kuweza kufanya vizur Kama jumuiya hiyo. Kwa nafasi yake atakuwa tayari kuwapa ushirikiano kwa UWT -Njombe ili kuweza kusaidiana kuziimarisha jumuiya nyingine kwani anaamin zaidi katika ushirikiano.

 Endapo jumuiya zitaimarika basi ccm itakuwa haina sababu ya kushindwa, tutaendelea kushika dola na kushinda.

Nyota huyo mzaliwa wa ludewa siku hadi siku ameonekana kuiteka anga ya siasa kwa namna ambavyo anawajibika katika nafasi yake aliyonayo kisiasa, kwa kuanza vyema majukumu, huku akizikacha kauli zisizo kuwa na uwezo wa kuisaidia jumuiya hiyo kwani anaamn bila kushirikiana hatuwez kufikia mipango ya UWT. 


Imetolewa na the titho stambuli na Mtokoma na Erasto k kizumbe ....kutoka ofisi ya siasa na uenezi Mkoa wa Njombe.

Maoni